December 8, 2017




Kikosi cha Azam FC kesho kinashuka dimbani kuwavaa Friends Rangers katika mechi ya kirafiki.

Mechi hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Azam FC imeamua kuivaa Friends Rangers kwa ajili ya kuendelea kujiweka fiti kabla ya Ligi Kuu Bara.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema kila kitu kiko tayari kwa ajili ya mechi hiyo.


“Maandalizi yamekamilika na mechi itachezwa saa 1 jioni na kutoa nafasi kwa watu wengi kuhudhuria,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic