December 8, 2017




Mashabiki wa soka nchini watapaa nafasi ya kumuona mshambuliaji mpya wa Azam FC, Bernard Arthur.

Arthur raia wa Ghana ataanza kuichezea Azam FC kesho katika mechi ya kirafiki dhidi ya Friends Rangers.

Mechi hiyo itakuwa ya kwanza kwake na Azam FC imeamua kuandaa mechi ya kirafiki ili kujiweka vizuri kabla ya kuendelea kwa Ligi Kuu Bara ambayo imesimama sasa.

Mghana huyo amesajiliwa kutoka Klabu ya Liberty Proffessionals ya nchini Ghana akichukua nafasi ya Mghana mwenzake, Yahaya Mohammed aliyefungashiwa virago hivi karibuni.

Msemaji wa Azam FC, Jaffer Iddi Maganga amesema, Arthur amekuwa akishirikiana vizuri na wenzake na anaonekana kuzoea mapema hali ya hewa na mazingira.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic