December 16, 2017
Simba imeamua kumaliza utata wa usajili usiku wa manani baada ya kuwasajili Dayo Domingues na Sante Kwasi katika nafasi zao za wachezaji wa kimataifa.

Awali kulikuwa na utata mkubwa kwa mchezaji Kwasi, kwani pamoja na Simba kuwa naye jijini Dar es Salaam kwa siku mbili, ilielezwa bado ana mkataba wa miezi saba na Lipuli FC.

Hali hiyo iliwapa hofu Simba ingawa wakala wa mchezaji huyo aliendelea kuhakikisha kwamba si kweli.

Simba ilikuwa na uhakika na Domingues aliyetokea Msumbiji lakini ikashindwa kumalizana na Kwasi hadi usiku wa manani ilipoamua kumaliza kasi.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV