Kocha wa Man City, Pep Guardiola ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Premier League mwezi Novemba.
Hiyo inamfanya kuingia kwenye rekodi ya kocha aliyeshinda tuzo tatu mfululizo za kocha bora wa EPL.
Kabla, Pep alikuwa anashikilia tuzo za Septemba na Oktoba kabla ya kuibuka mshindi tena.
Ushindi huo unamfanya awe kocha wa pili kupiga ‘hat trick’ ya tuzo za makocha EPL baada ya Antonio Conte wa Chelsea ambaye alifanya hivyo msimu uliopita.
Conte alishinda tuzo hiyo kuanzia Oktoba, Novemba na Oktoba mwaka 2016.
0 COMMENTS:
Post a Comment