Droo ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup – ASFC), imefanyika jana Jumatano Desemba 06, 2017 kwenye Studio za Kituo cha Televisheni cha Azam, kilichopo Tabata relini, Dar es Salaam.
Droo hiyo itakayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Mdhamini wa michuano hiyo – Kituo cha Televisheni cha Azam, ilichezeshwa na wachezaji wanne wa zamani wa Taifa Stars ya Tanzania, Mohammed Mwameja, Steven Names, Kanneth Mkapa na Bita John.
Michuano hiyo ambayo Bingwa Mtetezi ni Simba SC ya Dar es Salaam imepangwa kucheza na Green Warriors katika mchezo utakaopigwa ama Desemba 22, 23, 24 au 26.
Mchezo huo utakuwa ni wa uzinduzi rasmi wa michuano hiyo msimu huu kwa kuwa unahusisha bingwa mtetezi.
Kwa mujibu wa droo hiyo, JKT Mlale itacheza na KMC; Ambassador na JKT Oljoro; Mshikamano itacheza na Polisi Tanzania; Rhino ya Tabora na Alliance ya Mwanza; Ashanti na Friends Rangers za Dar es Salaam; Toto African ya Mwanza na Eleven Stars ya Kagera; Majimaji Rangeres ya Lindi na Mbeya Kwanza ya Mbeya; Milambo ya Tabora itacheza Buseresere ya Geita.
Nyingine ni African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Biashara ya Mara itacheza na Mawenzi Market ya Morogoro; AFC ya Arusha itacheza na Stand United ya Shinyanga; Lipuli ya Iringa na Burkina ya Morogoro; Mvuvumwa na JKT Ruvu; Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma; Polisi Dar itapambana na Mgambo JKT ya Tanga.
Mechi nyingine zitakuwa ni kati ya Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar ila kwa sasa imeweka maskani Shinyanga; Shupavu na Real Mojamoja; Mufindi United na Pamba ya Mwanza wakati Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani itacheza na Madini FC ya jijini Arusha.
Abajalo itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons; Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma; Bodaboda FC ya Singida United; Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation; Boma FC na Ndanda; Simba na Green Worriers; Area C na Azam FC; Young Africans na Reha zote za Dar es Salaam; Ihefu na Mbeya City; Mtibwa Sugar na Villa Squad; Kagera Sugar na Makambako wakati Mbao itacheza na Makanyagio.
0 COMMENTS:
Post a Comment