December 8, 2017



Aliyekuwa  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, anatarajiwa kuagwa kesho Jumamosi katika Hospitali ya Jeshi la Lugalo jijini Dar kabla ya kusafirishwa kuelekea  Korogwe, Tanga kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika keshokutwa Jumapili.

Bendera alifariki juzi Jumatano kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupelekwa akiwa mahututi akitokea katika Hospitali ya Bagamoyo muda mchache kabla ya kuaga dunia.

Kiongozi huyo ambaye pia  ni mwanasiasa mkongwe na aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania iliyoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 1980.

Msemaji wa familia ambaye ni mdogo wa marehemu, Allen  Bendera alisema kuwa wanatarajia kuusafirishia mwili wa ndugu yao kesho Jumamosi kuelekea mkoani Tanga baada ya kuagwa kwenye Viwanja vya Hospitali ya Lugalo.

“Kwanza mwili wa marehemu tayari tumeshauhamisha kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kupelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kwa ajili ya kuhifadhiwa kwenye sehemu ya VIP kabla ya siku ya Jumamosi kuagwa na wadau wa michezo na viongozi.


 “Lakini tunatarajia kumsafirisha  siku ya Jumamosi kuelekea  Korogwe Tanga kwa ajili ya mazishi ambayo yatafanyika siku ya Jumapili baada ya ibada ya kumuombea itakayofanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Michael,” alisema Bendera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic