December 24, 2017





Kocha Joseph Omog ambaye ametemwa na klabu ya Simba, hakutaka kuachwa kwa beki mkongwe, Method Mwanjali.

Omog raia wa Cameroon, pia imeelezwa hakutaka kusajiliwa kwa beki mwingine wala kusajiliwa kwa beki Juuko Murshid raia wa Uganda kwa kuwa hakuona kama ana mchango mkubwa katika kikosi chake.

Rafiki wa karibu wa Omog ameiambia SALEHJEMBE kwamba pamoja na kocha huyo kufutwa kazi Simba, lakini kuna makosa mengi sana hayamhusu.

“Umeona hali ilivyo, wachezaji wamemuangusha na huenda wazawa wamechangia sana kwa kuwa si watu wanaojituma.

“Lakini kocha amekuwa hataki mambo mengi na hasikilizwi, hakumtaka Juuko kwa kuwa anaona hajitumi, muda mwingi yuko Uganda na akienda huko anachelewa, haonyeshi juhudi mazoezini na kwenye mechi.

“Kwa upande wa Mwanjali, yeye hakutaka aachwe, maana uchezaji wake bado aliamini una msaada. Pia Simba ina walinzi wengi vijana, ilikuwa rahisi kuisaidia Simba wakiwa na beki mzoefu kama Mwanjali.

“Lakini ameachwa, Juuko asiyemtaka amesajiliwa. Leo timu imefanya vibaya yeye ndiye mwenye lawama. Kuna mchezaji kutoka Msumbiji, naye amesajiliwa, aliomba angalau aone video yake tu, hakutumiwa hadi anafika hapa,” alieleza rafiki yake huyo.

Tayari Omog ameishapewa taarifa ya kufutwa kazi baada ya Mohamed Dewji ‘Mo’ kuandika mtandaoni kuwa hana uwezo lakini angemshauri Omog kupumzika.



Hii ilikuwa ni baada ya timu hiyo kufungwa kwa mikwaju 4-3 ya penalti na kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho na Green Worries inayoshiriki Ligi Daraja la Pili.

1 COMMENTS:

  1. Kwa kuchangia tu. Watanzania ni watu wenye maneno mengi sana na mengi kati ya maneno hayo wakati mwengine yanakera hata kuyasikiliza. Kwa mfano kumuunga mkono Omog kumuacha Juko Murshidi zidi ya Mwanjali jamani? Kweli kocha mwenye kujitambua atakubali kumuacha mchezaji kama Juko ambae ni kijana wa mbali tu zidi ya Mwanjali? Juko ni beki panga pangua wa timu yake ya Taifa ya Uganda . Juko yupo fiti kabisa hasumbuliwi na majeruhi ukilinganisha na Mwanjali. Juko ni miongoni mwa wachezaji wachache walioitumikia simba kwa muda mrefu na naweza kusema kwa uadilifu mkubwa kwa sababu tumekuwa tukiwashuhudia wachezaji wakibongo wanaoitumikia simba wakiyumbishwa na tamaa zaidi kuliko michamgo yao kwa klabu wakitishia kuihama club hiyo mara sijui natakwa yanaga oh Azam lakini hatujawahi kumsikia Juko akipanua mdomo wake hovyo licha ya ukweli ni kwamba Juko ana uwezo wa kuchezea timu yeyote ile tena kwa mafinikio hata nje ya nchi.Ushauri wa Omog juu Simba kumuacha Juuko ni sawa na ushauri wa Phiri juu ya kuachwa Tambwe kwenda yanga. Watu wanashindwa kufahamu au kutouwelewa mchezo wa mpira na mikakati yake kwa sababu Simba hakuna sababu ya kutotwataa ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita. Ni uzembe pekee ndio uliopelekea Simba kuukosa ubingwa mwaka jana. Na tunapozungumzia uzembe basi kocha na bench lake ufundi haliwezi kukosa lawama. Lakini licha ya Simba kuimarisha kikosi chake kwa kumptia Omog wachezaji bora bado inaonekana makosa ya mwaka jana yaliyoihagharimu timu ua simba ubingwa yana kila dalili yakujirejea tena. Simba kumfukuza kazi Omog wamefanya maamuzi sahihi kabisa tena wamechelewa . Kama ningekuwa nina ushauri wa karibu ndani ya klabu ya Simba basi ningewashauri kumrejesha yule kocha walieshindwana nae kimalipo wakati ule hali ilipokuwa sio nzuri kiuchumi. Yule jamaa ni kocha hasa na aliipenda simba sidhani kama atakuwa hana kazi hivi sasa lakini kama yupo free simba wanapaswa kumrejesha kwa manufaa ya club na maendeleo ya mpira Tanzania. Kwanza ana uwezo wa hali ya juu ya kuinua ari ya wachezaji kitu ambacho Omog anakikosa kabisa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic