December 31, 2017


FULL TIME

Dk ya 94: Mwamuzi anamaliza mchezo, Mbao wanaendeleza rekodi ya kuifunga Yanga mfululizo, wanaibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Dk ya 90: Zinaongezwa dakika 4.

Dk ya 89: Mambo bado ni magumu kwa Yanga.

Dk ya 84: Yanga wanafanya shambulizi kali, Pius Buswita anashindwa kumalizia kazi nzuri waliyoifanya.

Dk ya 83: Upinzani umekuwa mkali.

Dk ya 80: Yanga wanapambana kutafuta bao la kusawazisha.

Dk ya 76: Beki wa Mbao, David Mwasa anapata kadi ya pili ya njano. Anatoka nje, sasa Mbao wako pungufu.

Dk ya 72: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Papi Tshishimbi anaingia Yusuph Mhilu.

Dk ya 68: Yanga wanaruhusu bao la pili baada ya walinzi kufanya uzembe.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 65: Mbao wanamtoa James Msuva, anaingia Boniface Maganga.

Dk ya 60: Mbao wanafanya mashambulizi makali mara mbili mfululizo.

Dk ya 57: Mwashiuya anaingia, anatoka Emmanuel Martine.

Dk ya 53: Mbao FC wanapata bao la kwanza kupitia kwa Habib Haji ambaye anapiga shuti kali la nje ya eneo la 18.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 50: Mchezo umekuwa na ushindani mkali.

Dk ya 47: Mbao wanatulia na kujipanga.

Dk ya 45: Yanga wameanza kwa kasi, Martine anafanya shambulizi lakini mpira unatoka.

Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO

Dk ya 45 + 49: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.

Dk ya 45: Zinaongezwa dakika nne za nyongeza.

Dk ya 42: Mbao wanafika langoni mwa Yanga lakini umakini wa walinzi unasaidia.
Dk ya 41: Tshishimbi anapiga shuti linapaa juu ya lango.

Dk ya 37: Kipa wa Mbao yupo chini anapatiwa matibabu baada ya kuumia.

Dk ya 34: George Sangida wa Mbao FC anapata kadi ya njano kwa kucheza vibaya dhidi ya Buswita.

Dk ya 28: Mbao bado wanaonyesha ubora wa kuwadhibiti Yanga.

Dk ya 25: Tambwe anafika langoni mwa Mbao lakini shambulizi lake linaokolewa.
 Dk ya 20: Mambo bado magumu kwa kila upande, wanapena zamu kumiliki mpira.

Dk ya 15: Mbao wanapata kona mbili mfululizo, zinapigwa lakini haziisumbui Yanga.

Dk ya 10: Yanga wameongeza kasi ya kushambulia. Wanatengeneza nafasi kadhaa.

Dk ya 7: Kasi ya mchezo imepungua.

Dk ya 5: Mbao wanapata kona inapigwa lakini haina madhara.

Dk ya 2: Yanga wanapata faulo nje ya 18, inapigwa inapaa.

Mchezo umeanza.

Timu zinapiga picha za kumbukumbu.

Timu zinaingia uwanjani. Mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Kumbukumbu tu ni kuwa Yanga imefungwa mara mbili mfululizo dhidi ya Mbao katika michezo yao miwili iliyopita kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

4 COMMENTS:

  1. Mwaka huu hyo yanga itatuaibisha sana. Wachezaji hawana viwango vya kucheza yanga, kocha uwezo mdogo. Timu ya watoto wasiojielewa. Pumbavuuuuu

    ReplyDelete
  2. Kwa hyo yanga kuchukua ubingwa labda kama mnategemea sangoma. Mnaacha musajiri wachezaji wanaojielewa mnang'ang'ania takatak ngoma na hao mababu akina tambwe,kamusoko. Hanna timu hapo

    ReplyDelete
  3. Yanga waliwafanyia ufidhuli na kehelu ya juu mbao. Aibu gani hii kulala mbili sufuri na huku Mbao wakicheza wapungufu

    ReplyDelete
  4. Hahahahah uku kwetu Furaha tu

    Happy New Year #MbaoFc

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic