December 7, 2017






Kikosi cha Yanga kimepewa mapumziko ya siku moja baada ya kufanya mazoezi kwa siku tatu mfululizo.

Kocha George Lwandamina ameamua kikosi hicho kipumzishwe baada ya mazoezi ya siku tatu mfululizo kuanzia Jumatatu.


Yanga ilianzia mazoezi yake gym kwa siku mbili na Jumatano wakafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru.

Taarifa za kutoka Yanga zinaeleza wataendelea na mazoezi kesho baada ya mapumziko ya leo.

“Kocha alimueleza meneja leo tupumzike, maana tumefanya mazoezi makali mfulilizo na mechi haziko mbali,” kilieleza chanzo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic