December 30, 2017




MPIRA UMEKWISHAAAAA
-Wanachofanya Simba sasa ni kuziba nafasi wanapokuwa hawana mpira lakini wanapoupata wanauchezea kuhakikisha wanabaki nao ili kuizuia Ndanda kuwashambulia

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 90, Simba wanagongeana vizuri lakini mwisho Kitandu anashindwa kuwa makini, goal kick
Dk 88 sasa, Simba wanaonekana kucheza mpira taratibu wakipoteza muda kama wameridhika


Dk 81, Mponda anatumia uzoefu wake kuachia mkwaju mkali lakini hakulenga lango. Goal kick
Dk 78, Ndemla tena anaamua kuachia mkwaju mkali kabisa hapa, hakulenga lango
Dk 76, Ndanda wanagongeana vizuri kabisa zaidi ya pasi saba lakini mwisho mpira unaishia mikononi mwa Manula
Dk 73, shambulizi jingine la Simba lakini inakuwa goal kick. Bocco alijaribu hapa
SUB dk 72 Alex Joseoh anaingia kuchukua nafasi ya John George upande wa Ndanda
SUB Dk 72 Simba wanamtoa Kotei nafasi yake inakwenda kwa Yusuph Mlipili


Dk 68, Ndanda wanafanya shambulizi kali lakini shuti la Mponda linaokolewa, Ngassa anapiga shuti udenda na Simba wanaokoa
Dk 65, shambulizi jingine la Simba, Ndemla aanachia mkwaju wake mkali wa tatu, goal kick
Dk 64, Kitandu anapata nafasi nzuri lakini anaachia shuti mtoto
SUB Dk 62, Koja anakwenda benchi upande wa Ndanda anaingia Omary Mponda
Dk 61, Koja wa Ndanda anajaribu shuti kali lakini goal kick 
Dk 59, Ndemla anaachia mkwaju mwingine mkali hapa, goal kick


GOOOOOOOOOO Dk 56 Kitandu anauacha mpira, unampira Beki na Bocco anauwahi na kuukwamisha wavuni, Simba mbili
Dk 55, Ndemla anaachia mkwaju mkali nje ya 18, kipa Kisubi anadaka unamtoka lakini anauwahi tena
SUB Dk 53 Simba inamtoa Liuzio na nafasi yake inachukuliwa na Kitandu (huyu ni nahodha wa zamani wa timu ya vijana ya Simba)
GOOOOOOOOO Dk 52, kona ya Kichuya, Bocco anaruka juu kama ndege ya kivita ya jeshi na kupachika bao


 Dk 51, Simba wanasukuma shambulizi na kupata kona ya nne ya ya kwanza katika kipindi cha pili
SUB Dk ya 51 Ndanda inamtoa Abdallah Selemani, Nafasi yake inachukuliwa na Ayoub Masoud
Dk 48, Ngassa anaachia mkwaju wa faulo lakini nyanyaaa kwa Manula
Dk 47 George anawatoka vizuri wachezaji wa Simba, anawekwa chini
Dk 46, pasi ya Ndemla, Bocco anageuka na kuachia mkwaju mkali hapa, nyanya kwa kipa
Dk 45 Mpira umeanza kwa kasi na kila upande unaonekana umepania kutengeneza matokeo bora katika kipindi cha pili




MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, Simba wanapata kona yao ya tatu ya mchezo, inachongwa lakini haina faida kwao
Dk 43, kona inachongwa, wachezaji wawili wa Ndanda wanapiga mashuti mawili mfululizo lakini mwisho ni goal kick, ilikuwa hatari katika lango la Simba ambao sasa wamepoteza mwelekeo
Dk 42, shambulizi jingine la Ndanda, Ngassa anamzidi kasi inakuwa kona

SUB Dk 42 Mo Ibrahim anakwenda benchi kwa upande wa Simba na nafasi yake inachukuliwa na Said Hamis, Ndemla Dk 41 krosi safi ya Bukaba, Liuzio anautoea lakini mwamuzi anasema ameotea
Dk 40 mpira wa adhabu katika lango la Ndanda lakini si shambulizi kali
Dk 38, mpira unaendelea kuchezwa katikati ya uwanja na mashambulizi dhaifu
KADI Dk 34 Koja wa Ndanda anaonywa kwa mdomo na mwamuzi kwa kucheza faulo 
Dk 33, inachongwa kona nyingine hapa lakini Simba wanaokoa kupitia Bocco
Dk  32, Ngassa anaingia vizuri lakini katika kuokoa, Nyoni anautoa na kuwa kona, inachongwa Simba wanaokoa, kona ya nne ya Ndanda, Simba wana moja



Dk 31, Kichuya anaokoa vizuri na kutoa pasi kwa Liuzio lakini anawekwa chini
Dk 28, Manula ameamka, kosa safi inachongwa lakini Simba wako makini, wanaokoa
Dk 27 sasa, Manula bado yuko chini akiendelea kupatiwa matibabu
Dk 25 Manula bado yuko pale chini akipatiwa matibabu
Dk 24, shambulizi kali la mechi hadi sasa, Ndanda wanapasiana na kuipenya ngome ya Simba, Jacob Massawe yeye na Manula ambaye anaokoa na Bukaba akaokoa na kuwa kona nyingine ya Ndanda


Dk 23, shambulizi jingine la Simba, Bocco anampasia Muzamiru, anaachia mkwaju mkali lakini goal kick
Dk 22, Ndanda wanafanya shambulizi kali la kwanza, pasi ya Ngassa, George anaachia shuti safi linazuiliwa na kuwa kona ya kwanza ya Ndanda, inachongwa lakini ni goal kick
Dk 20, Simba wanapata kona ya kwanza, Kichuya anaichonga ndani lakini Ndanda wanaokoa na kufanya shambulizi safi
 Dk 18 sasa, mpira umechangamka, zaidi unachezwa katikati ya uwanja, hakuna mashambulizi makali na Ndanda wanaonekana kama kuwatuliza Simba
Dk 13 Mo Ibrahim anaingia vizuri na kuachia shuti ndizi, mpira unatoka sentimeta chache katika lango la Ndanda


Dk 12 sasa, Simba wanaendelea kusukuma mashambulizi mfululizo katika lango la Ndanda lakini bado hakuna umakini katika umaliziaji
Dk 8, krosi saafi ya Kichuya ndani ya lango la Ndanda FC, mwamuzi msaidizi ananyoosha kibendera
Dk 7, inaonekana Ndanda hawana shambulizi kali hata moja na Simba wanatawala katikati ya uwanja na kufikisha mashambulizi
Dk 5, Majid Hamisi wa Ndanda anajaribu shuti baada ya kupokea pasi ya Mrisho Ngassa lakini anabutua juuu
Dk 4, Bocco anaingiza krosi nzuri baada ya kuiwahi pasi ya Kotei, lakini Liuzio anashindwa kuuthibiti
Dk 3, Bocco peke yake anapokea pasi nzuri ya Kichuya katikati ya lango, anatoa nje
Dk 1, Simba ndiyo wanaanza kwa kasi kubwa lakini mabeki wa Ndanda wako makini

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic