December 30, 2017




 Ili kuituliza Mbao FC licha ya kuwa kwao, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, walianza mikakati mapema kabisa.

Yanga ilifanya kila linalowezekana na maandalizi ya mchezo huo yalianzia kwa viongozi wa timu hiyo Tawi la Mwanza nao wameandaa mikakati ya kuwazima wapinzani wao.

Mbao kesho Jumapili itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa. Msimu uliopita Yanga ilifungwa bao 1-0 katika mchezo wa ligi hiyo uwanjani hapo.

 Katibu Mipango wa Tawi la Yanga Mwanza, Hashim Omar amesema wameandaa mikakati kabambe ya timu yao kushinda.

“Tunajua Mbao ni timu nzuri na inakuwa na uwezo mkubwa inapokuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani lakini kuelekea mchezo wetu, hatutaruhusu kufungwa tena.

“Tumejipanga kuvunja mwiko wa kutowafunga Mbao kwenye uwanja wao wa nyumbani, tumejiwekea mikakati ambayo tunaamini Yanga inashinda pale,” alisema katibu huyo.

Omary akiwatoa hofu Mbao, alisema wao kama viongozi wanaamini katika sheria 17 hivyo hawajaandaa mkakati wa nje ya uwanja ili kushinda.

Wakati huohuo, Yanga katikati ya wiki hii ilitanguliza kundi la viongozi na wanachama wake jijini Mwanza kuhakikisha wanaweka mazingira sawa kabla ya mchezo wao dhidi ya Mbao.


Kikosi cha Yanga kilitarajiwa kuwasili Mwanza jana kwa ndege kutoka Dar es Salaam na kilifanya mazoezi ya mwisho juzi asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic