December 8, 2017



Simba imeichapa KMC kwa mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, usiku huu.

Mechi hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya kujiweka sawa kwa timu zote na mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco na mshambuliaji Jonas Sakuwaha raia wa Zambia.

Mshambuliaji huyo anawania nafasi ya kusajiliwa Simba na alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza likiwa la pili kwa Simba kabla ya Bocco kupigilia msumari wa mwisho.

KMC walianza kupata bao kupitia Reyman Mgungila katika ya saba tu na kwa upande wa Simba, Bocco ndiye alianza kufunga bao katika dakika ya 16 na Sakuwaha akafunga la pili katika dakika ya 39. Kipindi cha pili, Bocco alifunga lake la pili na la tatu katika mechi hiyo.

KMC inayofundishwa na Fred Minziro, mara kadhaa ilijitutumua na kuonyesha soka safi lakini ilikuwa na tatizo kubwa katika umaliziaji.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic