Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Yanga kimerejea mazoezini tena, safari hii kikianzia gym.
Yanga wameanza mazoezi leo wakijifua kupitia gym na kesho wanatarajia kurejea uwanjani.
Wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja baada ya sare ya bila kufungana katika mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania.
Pamoja na sare, Yanga walionekana kufarijika baada ya wachezaji wake wawili, kiungo Papy Tshishimbi na Mrundi, Amissi Tambwe kurejea uwanjani na kucheza mechi tena.
Yanga imekuwa ikisumbuliwa na majeruhi mfululizo lakini kocha George Lwandamina amekuwa akipamba kuhakikisha wanakuwa katika mwendo mzuri.
Kwa kweli viongozi yanga mtuombe radhi mashabiki. Hamuwezi jitokeza media eti kujisifu mmemsajiri nkomola na huyo fiston then tutegemee tukapambane na timu kubwa kama Tp mazembe, hao mababu tambwe na ngoma ni kama tairi lenye vraka kamwe huwezi safiri ukilitegemea ktk safari ndefu. Bora hata timu isishiriki club bingwa afrika kuliko kutupa aibu na hyo timu isiyo hata na sub wa maana. Eti tuamini mwashiuya ataweza pambana na beki za zamalek au etoil du sahil. Tunajidanganya tu. Kama tulishindwa Mwaka Jana japo kikosi kilikuwa kikubwa eti tuweze Leo kwa kumtegemea chrwa na ajibu! Nina hakika huu Mwaka tujiandae nasi kuwa wa matopeni maana cdhani kama kuna kombe tutapata
ReplyDelete