December 23, 2017



Benchi la ufundi la Yanga halikuwa limepanga kumtumia kipa wake namba moja Rostand Youthen katika mchezo wa kesho wa Kombe la FA dhidi ya Reha FC, lakini amerudishwa kikosini kwani makipa wenzake wote ni majeruhi.

Kipa Beno Kakolanya ambaye alitarajiwa kucheza mechi hiyo, yeye anasumbuliwa na malaria wakati chipukizi Ramadhan Kabwili yeye anasumbuliwa na maumivu ya tumbo. 

Makipa hao jana hawakufanya mazoezi na badala yake Rostand alifanya mazoezi na kipa wa kikosi cha vijana Mussa Mbise. 

Chini ya wasaidizi wa Kocha Mkuu George Lwandamina, ambao ni Noel Mwandila na Shadrack Nsajigwa, Rostand alionekana akifanya mazoezi na Mbise aliyeonyesha kiwango cha kuridhisha kuwa kipa wa akiba.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema kuwa: “Kabwili na Kakolanya wote wanaumwa ndiyo maana hawapo mazoezini. Kabwili anaumwa tumbo na Kakolanya anasumbuliwa na malaria.”

Saleh alisema, kiungo mshambuliaji Geofrey Mwashiuya naye ni majeruhi baada ya juzi Alhamisi kuumiza goti.


Wakati huohuo, Lwandamina alishindwa kuwasili juzi baada ya kuchelewa ndege na badala yake atawasili nchini leo Jumamosi kutoka kwao Zambia.

SOURCE: CHAMPIONI.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic