December 16, 2017




 Beki Fistoni Kayembe raia wa DR Congo analazimika kufanya kazi ya ziada na kumshawishi Kocha George Lwandamina ili kuwaweka benchi wengine.

Lakini beki kisiki hasa wa Yanga, Kelvin Yondani amesisitiza hawezi kuwekwa benchi kwa kuwa anauamini uwezo wake.


Hadi usajili wake unafanyika, Kayembe aliyeletwa Yanga na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi alikuwa chaguo la pili mbele ya Vincent Bossou aliyeondoka klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu.

Usajili wa Kayembe ulifanyika baada ya milionea mmoja mwanachana wa Yanga kufanikisha usajili wa beki huyo.

Yondani amesema kwa upande wake hakuna beki yeyote atakayekuja Yanga na kumuhofia kwamba atamuweka benchi.

“Mabeki wengi wamekuja na kuondoka Yanga na hakuna yeyote aliyeniondoa katika kikosi cha kwanza, siri kubwa kwangu ni kuheshimu mazoezi na kufuata miiko ya uchezaji,” alisema Yondani.


Hata hivyo, kuna uwezekano Yondani akacheza sambamba na Kayembe katika beki ya kati na kuwaacha benchi Andrew Vincent ‘Dante’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic