December 15, 2017



Simba inaonekana kama imekwama kumsajili beki Asante Kwasi.

Taarifa zinasema, Simba imegundua Kwasi ana mkataba wa miezi saba na Lipuli ya Iringa, jambo ambalo limewakatisha tamaa.

Simba ilikuwa imemficha Kwasi jijini Dar es Salaam kusubiri kumalizana naye baada ya wakala wake kusema hakuwa na mkataba na Lipuli.

Lakini baada ya kufanya uchunguzi wa kina kupitia kamati yake ya usajili, iliamua kufunga breki ili kutafakari kwanza kuangalia kama inawezekana kujadiliana na Lipuli au kuachana naye.

Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa saa sita na dakika moja, na inaonekana umebaki muda mchache Simba kumaliza na Lipuli ingawa ilielezwa kuna juhudi zilikuwa zinafanywa.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic