December 25, 2017




Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Yanga unaonekana kukerwa na kutorejea mapema kwa beki wao, Fiston Kayembe raia wa DR Congo ambaye alienda kwao lakini hadi jana Jumapili asubuhi alikuwa hajarejea akiwa amepitiliza muda aliopewa.

Kayembe aliyesajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili lililofungwa hivi karibuni akitokea Balende FC ya DR Congo, kwa mkataba wa miaka miwili, aliruhusiwa na uongozi wa timu hiyo kurejea kwao Congo kwa ajili ya kwenda kutatua matatizo ya kifamilia lakini mpaka jana asubuhi hakuwa amerejea.

Chanzo kimesema,  Mcongo huyo anawaumiza vichwa viongozi hao kutokana na kitendo chake cha kuwa kimya kurejea kuichezea timu hiyo licha ya muda ambao alipewa kwenda kwao kuisha tangu wiki iliyopita.

“Unajua kwamba huyu Kayembe ambaye tulimsajili hivi karibuni amewafanya viongozi waumie vichwa kwani tangu aliporuhusiwa kwenda kwao mpaka leo bado hajarejea licha ya kwamba anajua muda wake umeshaisha na anatakiwa awe amerejea.

“Na kitu kibaya ni kwamba hajatuma taarifa yoyote ile kwa viongozi ya kuonyesha kwa nini amechelewa ingawa alipoondoka hapa alienda kwenye matatizo ya familia yake, mpaka sasa haijulikani ni kipi ambacho kinamuweka huko lakini atakaporejea kila kitu kitajulikana,” kilisema chanzo hicho.


Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh ambapo alisema: “Hilo suala lipo kwenye uongozi, mimi sihusiki nalo ila mchezaji huyo hajafika mazoezini.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic