January 5, 2018



Ukisema kuwa amewanyamazisha pia ni sawa maana Joh Raphael Bocco amekuwa akionyesha kiwango bora dhidi ya wale waliokuwa wakiamini kuwa hana msaada.

Kiwango anachoendelea kukionyesha mshambuliaji, John Bocco kimetosha kwa Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Mrundi, Masoud Djuma kumpa unahodha mkuu nyota huyo.

Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu mshambuliaji huyo aifungie mabao muhimu katika mechi dhidi ya Ndanda FC iliyochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na matokeo kumalizika kwa Simba kushinda mabao 2-0.

Bocco anapewa cheo hicho cha nahodha mkuu akimrithi beki Mzimbabwe, Method Mwanjali aliyesitishiwa mkataba wake katika usajili wa dirisha dogo ambalo lilifungwa Desemba 15, mwaka huu.

Djuma alisema awali kabla ya kumpa cheo hicho, alikuwa ni nahodha msaidizi wa timu hiyo akisaidiana na beki wa kushoto, Hussein Mohamed ‘Zimbwe Jr’.

Djuma alisema anafurahishwa na kiwango cha Bocco anayecheza vizuri kwa kufuata maelekezo yake ambayo anampa kabla na baada ya mechi katika kuhakikisha anatimiza majukumu ya kufunga mabao.

“Nimempa cheo hicho cha unahodha mkuu kutokana na nidhamu yake ya ndani na nje ya uwanja, pia jinsi anavyotimiza majukumu yake akiwa uwanjani kwa maana kufunga mabao na kiwango kizuri anachokionyesha,” alisema Djuma.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic