January 5, 2018


Rais mpya wa Liberia, mwanasoka wa zamani, George Weah amemualika Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger katika hafla ya kuapishwa kwake Januari 22, mwaka huu.

Weah alikuwa mshambuliaji wa AS Monaco ya Ufaransa akiwa chino ya Kocha Wenger kati ya mwaka 1988 na 1992.


Mshambuliaji huyo nyota wa zamani wa AC Milan na Mwafrika pekee kuwa mchezaji bora wa dunia, alishinda uchaguzi wa Liberia kwa kura asilimia 61.5.

Hata hivyo, wako wamekuwa wakisema huenda Wenger atashindwa kwenda katika hafla hiyo jijini Monrovia kwa kuwa Arsenal itakuwa na kibarua cha kuivaa Crystal Palace Januari 20 na siku mbili baadaye yaani Januari 24 watakuwa dimbani kukipiga na Chelsea katika mechi ya pili ya nusu fainali ya EFL Cup.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic