January 21, 2018




Azam FC imeendelea kupambana baada ya kurejea katika msitari wa ushindi ikiitwanga Prisons kwa mabao 2-0.

Pamoja na kuwa ugenini kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Azam FC imeweza kuandika ushindi ikifunga mabao yake yote mawili katika kipindi cha pili.

Bao la kwanza la Azam lilipatikana katika dakika ya 70 kupitia beki wake, Yakubu Mohamed.

Wakati Prisons wakipambana kusawazisha, Paul Peter aliandika bao la pili katika dakika ya 81 na kuihakikishia Azam FC pointi tatu.


Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi 30 na kupaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara na Simba wanaocheza ugenini dhidi ya Kagera kesho, wako nafasi ya pili wakiwa na pointi 29.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic