Kiungo mwenye kasi wa Simba, Emmanuel Okwi amerejea nchini na leo amejiunga na kikosi cha vinara hao wa Ligi Kuu Bara.
Okwi amejiunga na kambi ya Simba iliyo mjini Morogoro akitokea kwao Uganda.
Mganda huyo amekuwa nje ya Simba kwa takribani mwezi na ushee wakati akiwa majeruhi.
Okwi ndiye kinara wa ufungaji mabao Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa na mabao nane licha ya kuwa nje ya kikosi kwa muda mrefu.
Okwi ndiye kinara wa ufungaji mabao Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa na mabao nane licha ya kuwa nje ya kikosi kwa muda mrefu.
Awali ilielezwa kwamba alitaka kurejea nchini lakini Kocha Masoud Djuma akamtaka kubaki Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment