January 24, 2018



Waamuzi kutoka Sudan Kusini wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Simba ya Tanzania na Gendarmerie Tnale ya Djobouti itakayochezwa Februari 21,2018 Uwanja wa Taifa.

Mwamuzi wa kati atakuwa Alier Michael James akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Suleiman Gassim ,mwamuzi msaidizi namba mbili Gasim Madir Dehiya wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Kalisto Gumesi Simon Samson na Kamishna wa mchezo huo kutoka Botswana ni Mmonwagotlhe Edwin Senai.

Mchezo wa marudiano utakaochezwa Djibouti kati ya Februari 20 na 21,2018 wenyewe utachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi na Kamishna wa mchezo atatokea nchini Rwanda.


Mwamuzi wa kati ni Eric Manirakiza akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Pascal Ndimunzigo,mwamuzi msaidizi namba mbili Willy Habimana,mwamuzi wa akiba Pacifique Ndabihawenimana na kamishna Gaspard Kayijuka.

2 COMMENTS:

  1. Kwa hiyo mchezo wa 1 februari 20 na marudiano kati ya februari 20 na 21, ama kweli Seleh Jembe,kazi unayo!!!!

    ReplyDelete
  2. Mchezo wa kwnza Feb 21 dar mchezo wa marudio Feb 20 au 21 mwaka huu huu 2018!! Mwandishi jaribu kuwa making unatuchanganya.Huwa hakuna uhariri kwenye blog?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic