January 21, 2018




Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali ataendelea na ziara katika mkoa wa Tanga kuwahamasisha wanachama kuunga mkono uongozi ulio madarakani.

Dalali maarufu kama Field Marshal, amesema anakwenda Tanga ambako atatembelea Tanga mjini pamoja na Pangani.

“Lengo ni kuzidisha nguvu ya umoja ndani ya Simba lakini pia kuwasisitiza wanachama na mashabiki kuunga mkono uongozi ulio madarakani.

“Uongozi ulio madarakani unahitaji umoja na sapoti ya wanachama na mashabiki. Nitakwenda kuzungumza na watu wa Tanga na baadaye Pangani,” alisema.


Dalali amekuwa akiafanya ziara hizo za uhamasishaji kwa kuwa ni mmoja wa viongozi wanaokubalika zaidi na matawi ya klabu hiyo na mara zote amekuwa akisisitiza suala la umoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic