January 22, 2018



Daktari Mkuu wa Simba, Yassin Gembe, amemruhusu beki kiraka, Shomari Kapombe kuanza kuichezea timu hiyo kwenye mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Hiyo ni siku chache tangu beki huyo apone majeraha ya nyonga baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu tangu aumie wakati akiitumikia Taifa Stars.

Beki huyo, hivi karibuni alianza mazoezi ya binafsi akiwa na timu hiyo ilipokwenda kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi. Yeye alikuwa akijifua kivyake.

Kocha msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma, alisema kuwa beki huyo hivi sasa yupo fiti kuanza kuitumikia timu hiyo.

Djuma alisema tayari ameanza kumuingiza beki huyo kwenye mipango yake ya mechi zijazo.

“Nikuhakikishie tu kuwa, Kapombe hivi sasa yupo fiti kwa ajili ya kuichezea timu yake ya Simba, kwani daktari Gembe tayari ametoa ruhusa ya kumtumia.

“Ujio wa Kapombe utaimarisha kikosi changu kwani nitakuwa na wigo mpana wa kuwatumia wachezaji wengi kutokana na aina ya mfumo ambao mimi ninataka kuutumia,” alisema Djuma.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic