Kocha Masoud Djuma amekubali kumkaribisha mshambulizi wake Emmanuel Okwi na kesho asubuhi ataanza mazoezi rasmi.
Tayari Okwi yuko katika kambi ya Simba mjini Morogoro ambayo ni maalum kwa ajili ya maandalizi kuivaa Singida United, Alhamisi.
Okwi ametua nchini leo na moja kwa moja ameungana na wenzake huko Morogoro.
Awali, Kocha Djuma alimtaka kubaki Uganda hadi atakapopona lakini alioenakana kutofurahishwa na uchelewaji wake.
Lakini taarifa zinasema, leo wamezungumza vizuri baada ya kuwasili Morogoro na kesho ataanza mazoezi rasmi.
0 COMMENTS:
Post a Comment