Arsenal hawajalala kama watu wanafikiria hivyo kwa kuwa wameamua kuziba pengo mara moja kama watamuuza Alexis Sanchez.
Kocha Arsene Wenger tayari amoeba kitita cha pauni milioni 60 kutoka kwa uongozi wa Arsenal ili kumnasa Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Mara kadhaa, Wenger amekuwa akionekana na nia ya kumnasa mshambulizi huyo lakini sasa sababu inaonekana kuwa kuu na angependa kumpata ili kuziba nafasi ya Sanchez kama atasajili na Manchester United au Manchester City.
Tetesi tumekuwa tukizisikia saana juu ya mchezaji fulani anatakiwa na Arsenal lakini mpaka dirisha linafungwa katika tetesi 10 labda 1 ndo itafanyiwa kazi,Kumpata Aubameyang kama mbadala wa Sanchez sioni kama itakuwa ndo mwisho wa matatizo pale Arsenal, tulifikiri hivyo baada ya kusajiliwa Lacazette lakini kila mtu anaona kinachoendelea pale Arsenal, bado timu ina udhaifu mkubwa sana hususan sehemu ya nyuma na viungo wakabaji, kwa sasa hivi pale Arsenal kiungo hasa mwenye asili ya ukabaji ni Elneny mana Coquelin ameshauzwa huko Spain.yaani kwa macho ya kawaida tu sio lazima uwe kocha wa mpira unaona kabisa kuna tatizo kubwa upande wa nyuma, hata kipa Cech tuliyeamini ni mmoja wa makipa bora Uingereza na Duniani sasa hivi anaonekana hamna kitu kwa sababu hapati ulinzi wa kutosha,maoni yangu Wenger asajili safu ya ulinzi iliyokuwa imara ikiongozwa na viungo wakabaji au wanaoweza kukaa na mipira muda mrefu kama mfano wa Barcelona wanaweza kujikwamua hapo walipo kuliko fedheha ambayo inapatikana, itafika mahali Arsenal itakuwa haipo tena kwenye ushindani na timu kama Chelsea, Liverpool,Man City na timu nyengine za top 6 na badala yake itakuwa inashindana na timu za chini kama tulivyoanza kuona mzunguko wa kwanza imefanikiwa kuifunga Tottenham tu kwa timu zilizo juu yake.Hayo ni maoni yangu tu.
ReplyDelete