January 12, 2018



Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, DPP ametoa maagizo mpya kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kufanya marekebisho ya upelelezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenzake inayosikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.

Malinzi anashitakiwa kwa makosa ya kughushi nyaraka zikiwemo risiti 20 za TFF pamoja na shitaka la utakatishaji fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 375,418 akiwa na washitakiwa wengine ambao ni aliyekuwa Katibu wa TFF,  Selestine Mwesigwa na Nsiande Mwanga ambaye alikuwa muhasibu wa shirikisho hilo.

Katika kesi hiyo inayosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri, upande wa mashitaka kupitia Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Leornad Swai, jana Alhamisi aliiambia mahakama kuwa tayari faili la Malinzi na wenzake lipo mikononi mwao baada ya kutoka kwa DPP ambaye ametoa maagizo mapya kwenye upelelezi wake.

Swai alidai kuwa faili hilo lipo mikononi mwa Takukuru kwa ajili ya kuendelea na upelelezi wa kesi hiyo baada ya kupokea maelekezo ya marekebisho kwenye upelelezi wa kesi hiyo kutoka kwa DPP, hivyo wanaomba wapangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa tena kesi hiyo.


Kutokana na hoja hiyo upande wa utetezi ambao ulikuwa ukiongozwa na mawakili, Abraham Senguji na Nehemia Nkoko haukuweza kupinga chochote kabla ya Hakimu Mashauri kuahirisha kesi hiyo hadi Januari 25, mwaka huu.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic