Uongozi wa Majimaji umefunguka umejipanga kuhakikisha unaondoka na pointi tatu dhidi ya Azam FC ndiyo maana umeamua kucheza michezo ya kirafiki kujiweka fiti zaidi.
Msimu uliopita timu hizo zilitoa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Majimaji na sasa Azam ipo nafasi ya pili ikiwa ana alama 26 huku wapinzani wao wakiwa na pointi 11 wakishika ya 11.
Meneja wa Majimaji ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya Sokabet, Godfrey Mvula alisema wameamua kujiimarisha zaidi ili watakapokutana na Azam iwe rahisi wao kuweza kupata pointi.
Kiongozi huyo alisema kwa sasa timu ipo kwenye maandalizi makali kulekea mchezo huo.
“Mchezo ujao tutakuna na Azam, ni mechi ngumu lakini kwa upande wetu tumepanga kuondoka na ushindi kwa sababu huu ndiyo wakati pekee wa timu yetu kufanya vizuri na kuwa kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi,” alisema Mvula.
Tangu Majimaji ipate udhamini wa Sokabet ambayo ni kampuni ya kubadhiri matokeo, imekuwa na mikakati mingi ya kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja.
0 COMMENTS:
Post a Comment