Baada ya kuifungia mabao mawili timu yake ya Yanga katika Kombe la Mapinduzi, mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi ameahidi kuendelea na moto huo katika Ligi Kuu Bara.
Mshambuliaji huyo ambaye hakuwa na nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga alifanikiwa kufunga mabao baada ya kuwafunga Mlandege mabao 2-1 yote yakifungwa na Mahadhi.
Alifunga mabao hayo ikiwa muda mfupi baada ya kuwaomba msamaha mashabiki wa timu hiyo kufuatia kushindwa kuonyesha kiwango kikubwa katika ligi kuu na mashindano mengine.
Mahadhi alisema anajifunza mengi kupitia michuano ya Kombe la Mapinduzi, hivyo anaamini kwa kupitia michuano hiyo atafanya vizuri atakaporejea katika ligi kuu.
Mahadhi alisema ligi kuu ni ngumu tofauti na watu wanavyotarajia hivyo kupitia Mapinduzi atashika na kufuata maelekezo ya kocha wake, Shadrack Nsajingwa na Noel Mwandila waliopo Zanzibar katika kikosi hicho kinachoshiriki Mapinduzi.
Mahadhi amesema mabao hayo aliyoyafunga yatamjengea hali ya kujiamini na kuendelea kufunga zaidi.
"Kiukweli ligi kuu ni ngumu tofauti na Mapinduzi, hivyo basi kwa kupitia michuano hii itanisaidia kunijenga hali ya kujiamini na kuendelea kufunga mabao.
" Nimepanga kasi hii kuendelea nayo ya kufunga, ninaamini ni mwanzo mzuri kwangu," alisema Mahadhi, mchezaji wa zamani wa Coastal Union.
0 COMMENTS:
Post a Comment