January 1, 2018



Benchi la Ufundi la Majimaji FC, limesema kuwa, kukosekana kwa nyota wake wanne kwenye mchezo wao wa juzi Jumamosi dhidi ya Mtibwa Sugar, ndiyo sababu kubwa iliyowafanya washindwe kupata matokeo mazuri na kuambulia kipigo.

Juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, Majimaji inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet, ilifungwa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru, alisema nyota hao ambao ni Seleman Selembe, Paul Mahona, Tumba Sued na Abdallah Salamba, hawakuwepo kutokana na matatizo mbalimbali.

“Kama wangekuwepo nyota wetu wote nadhani tungeweza kuibuka na ushindi, lakini kukosekana kwao kumesababisha tupate matokeo hayo mabaya.


“Kikubwa tunajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michezo yetu ijayo ili tuweze kuwa sehemu salama ambapo mwisho wa msimu tubakie kwenye ligi,” alisema Ndunguru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic