Baada ya Joseph Omog kufungashiwa virago ndani ya Simba na kuondoka haraka nchini kwenda kwao, mwenyewe amesema kwa sasa atapata muda mzuri wa kupumzika kuliko hapo awali.
Omog, raia wa Cameroon, ambaye wiki moja iliyopita alisitishiwa ajira yake ndani ya Simba kutokana na kile kilichoelezwa ni matokeo mabaya ya timu hiyo, baada ya kupewa stahiki zake zote, usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita alipanda ndege na kurejea kwao Cameroon.
Muda mfupi kabla ya kuondoka kwenye ardhi ya Tanzania, Omog amesema kuwa: “Kiukweli hivi sasa nitapata muda mzuri wa kupumzika, tena kwa amani kabisa tofauti na hapo awali.
“Kipindi kile nilikuwa nikienda mapumziko sikuwa na amani sana kwa sababu nilikuwa nawaza sana kazi hata kama nipo likizo, lakini baada ya kuondoka Simba, huu mwezi mmoja nitakaokaa bila ya kufanya chochote nitakuwa na amani sana.”
Ikumbukwe kuwa, siku chache kabla Omog hajatimuliwa, alikuwa amepewa likizo ya takriban mwezi mzima baada ya ligi kusimama kupisha michuano ya Kombe la Chalenji iliyofanyika Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment