January 23, 2018


Manchester City imeamua kumuongeza kiungo wake wa pembeni Kevin De Bruyne mkataba wa miaka mitano na nusu.

De Bruyne atakuwa akipokea mshahara wa jump ua pauni 350,000 kwa wiki sawa na ule anaolipwa Alexis Sanchez aliyejiunga na Manchester United akitokea Arsenal.

Lakini mgawanyo wa De Bruyne ni pauni 280,000 ya mshahara kwa wiki pamoja na bonas ya 70,000.

Kiungo huyo wa pembeni mwenye kazi alikuwa akiwaniwa kwa karibu na klabu maarufu duniani ya Real Madrid na inaonekana City wamefanya hivyo kuhakikisha anabaki.

Kwa mkataba huo, sasa De Bruyne atabaki Manchester City hadi mwaka 2023.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic