January 2, 2018


Unaweza kusema mashabiki wa soka hawana kauli moja baada ya baadhi yao kumsifia mshambuliaji wa Simba, John Bocco kuwa anajituma sana.

Baada ya Bocco kufunga mabao mawili wakati Simba ikiimaliza Ndanda FC kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, mashabiki hasa wa Simba wanaonekana kufurahishwa na mwendo wa Bocco.
Katika mijadala ya makundi mbalimbali pia kupitia mtandao wa Instagram, mashabiki hao wa soka wameonyesha kufurahishwa na Bocco.

Wengi wameeleza pamoja na kufunga lakini amekuwa akicheza kwa juhudi kubwa na inapaswa kuwa mfano kwa wengine,
Lakini wako waliosema, Bocco anaonekana ana malengo hata kuliko wachezaji wengi wa kigeni kwa kuwa hataki kufeli.
Wakati wakimwagia sifa kibao, siku chache zilizpita, mashabiki walikuwa wakilalama kwamba Bocco anaonekana kutokuwa na msaada.


Mara kadhaa, hadi uwanjani walikuwa wakipiga kelele kutaka Bocco ataolewe, madai kwamba hana msaada.

1 COMMENTS:

  1. Inawezekana kabisa yale makelele ya mashabiki waliokuwa wakimponda John Boko kuwa hajitumi hana msaada yamemuamsha Boko na kujituma zaidi na kuonesha hiki kiwango kizuri cha upambanaji alinacho sasa au alikuwa bado hajawa fiti kutokana na majeraha yaliokuwa yakimkabili. Watu wengi wanasema kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi za kiafrica zenye vipaji halisi vya soka lakini vinakosa kuendelezwa. Utasikia vijana wetu wana ndoto za kwenda kucheza ulaya. Ni vizuri kabisa lakini sio jambo rahihisi hivyo. Lakini inawezekana ikawa rahisi kwa vijana wa kitatanzania kwakuwa vipaji wanavyo wakizingatia nidhamu na kuacha tamaa ya kujipatia pesa ambapo wakati halisi kwa wao kupata kipato halisi kulingana na uwezo wao haujafika au kuacha kukubali kurubuniwa na watu wanaojifanya wanataka kuwasidia wakati kiukweli ni kwamba hao watu hutaka kujisaidia wao wenyewe binafsi kwa kuwatumia hawa vijana na kuwapelekea wakati mwengine kuwatia matatizoni na vilabu amabavyo vingewafanya waonekane au hata kuwatoa nje ya nchi . Kuchukua au kuomba ushauri kwa wachezaji walioyocheza nje ya nchi kwa mafinikio ni moja ya elimu muhimu kwa wachezaji wetu hasa vijana. Kwa kuwa Tanzania hatuna watu wa namna hiyo wa kutosha kwa hivyo moja kwa moja Mbwana Samata anakuwa mtu sahihi kabisa kwa wachezaji wetu vijana kuomba ushauri ikiwa wao wenyewe au watu makini wanaowasimamia lazima wawe na contact na Samata sio kumuomba hela bali kumuomba utajiri nasaha wa soka alionao, nadhani hata Mbwana atajisikia fahari. Unakumbuka Khassani Mgosi aliwahi kumuuma sikio John Boko kwamba akiongeza bidii kidogo tu basi hakuna fowadi wa kumshika kwenye ligi. Inakuwaje Amisi Tambwe awe bora kuliko John Boko tena kwa magoli ya vichwa? Wakati John Boko ni mwepesi na anakimo kirefu sihaba. Kitu kimoja utagundua kutoka kwa Amisi Tambwe ni mwili uliojengeka hasa kimazoezi kitu ambacho kinakosekana kwa wachezaji wetu wengi wa kitatanzania. Nguvu na utimamu wa mwili unakamilisha utimamu wa akili kwa mchezaji kufanya kile nachotaka kufanya uwanjani.
    Kheri za mwaka mpya kwa wote.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic