January 27, 2018



Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amefunguka kuwa, amemuandaa ipasavyo beki wake Juma Nyosso kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Lipuli FC utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Kaitaba.

Kawaida Nyosso ambaye ni beki mzoefu hucheza namba tano au kitasa cha timu kuhakikisha hakuna hatari langoni mwake akishirikiana na Mohamed Fakhi, wote waliwahi kucheza Simba.

Jumatatu iliyopita, Nyosso alikumbana na kadhia baada ya kumshambulia shabiki wa Simba, Shabani Hussein (23) mfanyabiashara ndogondogo ambaye alizimia na kukimbizwa hospitali baada ya kumchokoza kwa kumpulizia vuvuzela sikioni.

Kufuatia tukio hilo, beki huyo alijikuta mikononi mwa polisi ambapo alilala siku moja kabla ya kuachiwa kwa dhamana siku ya Jumanne jioni.

Maxime alisema kuwa, beki wake huyo hana tatizo lolote la kushindwa kumtumia katika mchezo wake dhidi ya Lipuli na kudai kuwa atakuwa miongoni mwa wachezaji 11 watakaocheza mchezo huo.

“Nyosso hana matatizo yoyote ya kushindwa kumtumia katika mchezo wetu na Lipuli, hana jeraha lolote wala nini, ni mmoja wa wachezaji ninaowategemea katika kikosi changu.


“Shabiki ndiye alikuwa na makosa ya kumfuata mchezaji, mashabiki kama hao hawafai kwa kuwa wanafanya matendo ambayo si ya kiungwana,” alisema Maxime.

2 COMMENTS:

  1. Nchi yetu ni sehemu ya ajabu sana. Wanamichezo ni watu wenye mvuto katika jamii hasa kwa vijana wadogo wanaonyanyukia mara nyingi vijana wadogo huwahusudu na kuiga tabia za wanamichezo . Mwanamichezo licha ya kuwa binaadamu lakini hutakiwa kujitambua hasa anapokuwa katika halaiki ya watu na ndipo linapokuja neno professional. Kwa nchi za wenzetu wanaoheshimu nidhamu kwa wanamichezo mchezaji hata akaifanya makosa nje ya uwanja hasa ya udhalilishaji au k umdhururu mtu basi huwa hawana cha msalie mtume. Kitendo cha Juma Nyoso cha kutowajibishwa na Club yake au mamlaka yeyote ile inayohusika na masuala ya sheria au michezo na kumuachia aendelee na shughuli zake kama hakuja tokea lolote lile ni mambo ya hovyo na ya aibu katika michezo na hata katika maisha kama watanzania. Ni dhahiri kwa kutochukuliwa hatua yeyote Juma Nyoso kwa kumdunda yule shabiki ni kuwaruhusu watu wajichukulie sheria mikononi mwao na madhara ya kuwaachia watu wajichukulie sheria mikononi hovyo kila mtu anapofikwa na ghadhabu ni kuelekea kujenga jamii ya wahuni. Hata kama shabiki alitowa maneno ya shombo, Juma Nyoso kama professional alipaswa kutambua kuwa huyo alikuwa ni shabiki. Kama wachezaji wote waruhusiwe kuwa na mihemko ya mashabiki sijui kama amani ingekuwepo kwenye michezo. Kuanzia Club yake lazima walitakiwa kumuajibisha Juma Nyoso. Lakini cha kushangaza hakuna chama cha mpira cha wilaya au mkoa au hata taifa walioonesha kuwa serous na kosa la mtu aliekaribia kupoteza maisha ya mtu kwa ghadhabu zilizosababishwa na maneno matupu. Hayo maneno sijui jamaa alimpulizia vuvuzela sikioni ni upumbavu mtupu kwani juma nyoso alishadiriki kunyanyua mkono wake na kuupeleka sehemu za aibu kwa mwanaume mwenzake na laiti kama hao wachezaji wenzake aliowapapasa sehemu za aibu wangilikuwa wanakosa nidhamu kama yeye basi pangechimbika hapo hapo uwanjani. Kwa hivyo utaona ni ukosefu wa nidhamu uliompelekea Juma Nyoso kumjeruhi yule shabiki na kitendo cha kutothubutu kumuajibisha Juma Nyoso wakati bado kosa lipo moto ni kumpelekea ujumbe Juma Nyoso yakwamba alivyofanya ni sawa ila kuna watu fulani wanataka kukuonea.

    ReplyDelete
  2. Tunapoona chanzo cha tatizo ni jambo dogo basi tuna matatizo makubwa zaidi kwenye tasnia ya michezo kuliko tunavyoona. Shabiki akitetewa na kuonekana ubaradhuli wake ni jambo dogo na la kawaida lisilotaka kukemewa bali kufumbiwa macho na vyama vy michezo huku tukiviona v sidani kama tutakuwa tunajenga. Wenzetu wamekuwa wakiwafungia maisha mashabiki maandazi wenye ushabiki wa kijinga kama si kishamba maisha kwa sababu wanajua vyanzo vya vurugu na utovu wa adabu ni mashabiki. Ikumbukwe mashabiki wa Simba walivunja viti Uwanja wa Taifa na timu zikaadhibiwa badaa ya mashabiki!!! hivyohivyo tuangalie wenzetu Ulaya mara ngapi wamekuwa wakiwafungia mashabiki maandazi wenye mambo ya kishamba kama si kizamani kuingia viwanjani. Tunapaswa kukomesha vyanzo vya vurugu na si vurugu, ila kwa utashi na ushabiki wetu tunashabikia upuuzi tukijisahaulisha chanzo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic