January 27, 2018




Kampuni ya Matisun Group, inayoidhaini timu ya Ndanda FC, ya Mtwara kupitia bidhaa yake ya Kiboko, kesho inatarajia kuzindua mashindano ya mchezo wa Kriketi kwenye Uwanja wa Kawe jijini Dar es Salaam, ambapo timu zaidi sita zitaanza kuchuana katika hatua ya kwanza ya mashindano hayo .

Akizungumza kwenye kikao cha waandishi wa habari Meneja masoko wa kampuni hiyo Erhard Mlyans amesema kwamba wameamua kuelekeza nguvu yao katika mchezo wa kriketi ikiwa ni njia moja wapo ya kuongeza wingi wa michezo hapa nchini.



Amesema kuwa mwanzo walikuwa wakidili na mpira wa miguu pekee kwa kuidhamini Ndanda jambalo liliwafanya kujitangaza Zaidi.

“Tumejipanga kuongeza wigo wa michezo hapa nchini, kwani ili nchi ifahamike Zaidi kwenye mataifa mengine ni vizuri zaidi kuwa na  michezo ya aina mbalimbali hususani hii ya kriketi ambayo kwa namna moja haijaenea sana hapa nchini.


“Lakini tukiachilia mbali hivyo sisi tutaendelea kusapoti mpira wa miguu kwani tulianza na Ndanda FC, ila huko mbeleni tutaangalia timu gani nyingine nzuri ya kuisapoti ili lengo letu kama kampuni la kushirikiana na serikali kwenye michezo liweze kutimia maradufu,” alisema Mlyans.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic