January 27, 2018






MPIRA UMEKWISHAAAAAA

DAKIKA 3 ZA NYONGEZADk 90, Mahadhi anaipangua difensi ya Azam na kuachia mkwaju safi wa krosi lakini hakuna mtu katika nafasi


Dk 87, Azam wanagongeana vizuri lakini shuti la Hoza kazi bure
Dk 85, Yanga taratibu wanaanza kupoteza muda huku Azam FC wakiwa hawataki kupoteza hata senti ya muda
Dk 83, krosi nzuri ya Agyei, Mbaraka anaunganisha vizuri mbele ya Yondani, unatoka kidogo kabisa nje ya lango la Azam
KADI  Dk 81 Sure Boy analambwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumsukuma Kessy kama mzigo
Dk 80, Azam FC wanaonekana kugongeana vizuri lakini mipango yao ni duni ndani ya 18
KADI Dk 78 Morris naye analambwa kadi ya njano kwa kumrukia mgongoni Chirwa, inaonekana undava sasa umetawala zaidi


KADI Dk 76 Yondani naye analambwa kadi ya njano kwa kucheza kibabe dhidi ya Mbaraka na Agyei
KADI Dk 75 Tshishimbi analambwa kadi ya njano kwa ubabe, ni kadi ya kwanza ya YAnga leo na ya nne katika mchezo wa leo
Dk 73 Azam wanagongeana vizuri kabisa hapa lakini krosi ya Kangwa inatua mikononi mwa Rostande
Dk 72 Yanga wanapaswa kuwa makini katika eneo lao la katikati maana wanatoa nafasi nyingi za Azam kujaribu
Dk 71, Mbaraka anajaribu vizuri kabisa lakini Rostande anakuwa makini sana
SUB 68 Yanga wanamtoa Ajibu, nafasi yake inachukuliwa na Mahadhi
Dk 67 Himid Mao anajaribu mkwaju hapa lakini unakwenda nje


Dk 67, mkwaju wa faulo wa Agyei, Rostand anauwahi lakini anautema lakini anauwahi tena
SUB DK 66 Yanga wanamtoa Emmanuel Martin ambaye anaonekana aliumia, nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya
SUB Dk 65, Chilunda anakwenda nje upande wa Azam FC, anaingia Iddi
Dk 63, Azam ni zamu yao, lakini mpira wa Chilunda unawahiwa na Yondani, anaondosha hatari
Dk 62, Chirwa anajaribu kuingia vizuri lakini Morris anamdhibiti
Dk 60, Martin anawatoka mabeki wawili wa Azam, anagongeana na Ajibu vizuri lakini kipa Abarola anakuwa mjanja
Dk 57 Agyei katika nafasi nzuri kabisa, lakini anapiga shuti kuuubwa, goal kick


Dk 54, Azam FC wanaonekana kurejea katika hali yao, wanacheza vizuri katika eneo la katikati
Dk 51 sasa, bado mpira unachezwa muda mwingi zaidi katikati ya uwanja na hakuna timu iliyofungua mipango bora kupata bao la kuongeza au kusawazisha
SUB Dk 50 Azam FC wanamuingiza Mbaraka Yusuf ili kuongeza nguvu ya mashambulizi
Dk 49, Kangwa anamtoka tena Kessy na kumimina krosi safi kabisa, goal kick
Dk 46, Chirwa anawekwa chini na Nkongo anasema ni madhambi. Anaupiga vizuri Gadieal na Yanga wanaonekana kama wameanza kwa kasi nzuri
Dk 45, Yanga ndiyo wanaanza na kujaribu shuti lakini ni dhaifu


MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZAGOOOOOOOOOO Dk 44, shuti kali la Gadiel Michael linakwenda moja kwa moja wavuni baada ya kumshinda kipa wa Azam FC
KADI Dk 43 Kingu naye analambwa kadi kwa kumuangusha Makapu
Dk 42, shambulizi jingine zuri la Yanga lakini Razak anadaka vizuri mkwaju wa faulo wa Martin
Dk 39 Kangwa anamgongea mpira Kessy na kuwa kona, inachongwa tena na Kangwa inakuwa haina faida
SUB Dk 36, Azam FC wanamuingiza Salim Hoza kuchukua nafasi ya Benard Arthur
Dk 35, Martin anajaribu vizuri hapa, mpira wake unatoka juu kidogo ya lango la Azam  FC
Dk 33 mpira umesimama, Tshishimbi anatibiwa baada ya kugongana na Kingu



GOOOOOOOO Dk 30, Ajibu anatoa pasi nzuri kabisa kwa Chirwa anayeuwahi mpira mbele ya kipa wa Azam na kuukwamisha wavuni kwenye nyavu zilizo wazi
Dk 28, Ajibu akiwa mbali anajaribu vizuri kabisa, lakini kipa Abarola yuko makini kabisa
Dk 26, Azam FC inabidi wajihadhari kutokana na kucheza faulo nyingi mfululizo
Dk 24 Kessy anakwatuliwa na Kangwa mbele ya mwamuzi wa akiba, lakini anaonekana kama hakuona. Yuko nje anatibiwa
KADI Dk 22, Sure Boy analambwa kadi kwa kumuangusha Martin


Dk 20, Yanga bado wako katika lango la Azam, wanagongeana vizuri lakini Ajibu anapiga juu na kuwa goal kick
Dk 19, Yanga wanafanya shambulizi jingine zuri, Tshishimbi anagongeana na Ajibu na Chirwa anaachia mkwaju unatoka pembeni kidogo
Dk 17, Kangwa tena, anaingiza krosi nyingi nzuri, Yondani anaruka na kupiga kichwa anaondosha
Dk 16 Kangwa anamzidi tena ujanja Kessy, anaingiza krosi safi hapa, Yanga wanaokoa
Dk 15, Yanga wanagongeana vizuri kabisa, Tshishimbi anaachia mkwaju matata kipa Azam anadaka na kutema, lakini anauwahi tena


Dk 12, shambulizi jingine pole la Azam FC, Arthur anaachia mkwaju hapa lakini ni chakula kwa Rostand
KADI Dk 10, Chilunda anamkwatua Kessy na mwamuzi Nkongo anamramba kadi ya njano ya kwanza katika mechi ya leo Dk 7, Yanga tena, pasi nzuri ndani ya 18, lakini Tshishimbi anachelewa
Dk 5, Ajibu anajaribu mkwaju hapa lakini unakuwa dhaifu kabisa
GOOOOOOOOOO Dk 3, Kangwa anamtoka Kessy, anamtoka Raphael Daud na kuingiza krosi safi kabisa, Iddi anaunganisha na kuandika bao la kwanzaDk 2, Kessy anachuana vizuri na Kangwa na kumzidi maarifa, inakuwa goalkick
Dk 1, Yanga wanaanza na kufika katika lango la Azam FC, wanaokoa, nao wanaanza kushambulia kwa kasi


TAKWIMU ZAO KABLA YA LEO...
Zimekutana 31
Yanga shinda 12
Azam shinda 11
Sare 8

Yanga ilifunga mabao 41
Azam FC ilifunga mabao 40

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic