January 27, 2018



Beki wa kushoto wa Yanga, Gadiel Michael ambaye ameibuka shujaa wakati Yanga ikiizamisha Azam FC kwa mabao 2-1, amesema kilichomfurahisha ni namna alivyoweza kuisaidia timu yake kupata ushindi na si zaidi.

Gadiel amesema alitaka Yanga ishinde kwa kuwa ndiyo timu yake kwa sasa na si Azam FC. Mwisho amefanikiwa kufunga bao la pili wakati Yanga ikishinda kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, leo.

"Kikubwa ilikuwa ni namna ya kuitumia nafasi. Nimefanikiwa kufunga na kuisaidia timu yangu kushinda. Hili ndiyo jambo kubwa zaidi kwangu.

"Azam ni timu niliyotokea lakini sasa niko Yanga na nilikuwa nikiipiganie ishinde, mwisho tumefanikiwa," alisema.

Gadiel alipiga mkwaju wa takribani mita 25 uliomshinda kipa Razak Abarola raia wa Ghana na kuandika bao la pili la Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara, leo. 

Bao la kwanza la Yanga katika mchezo huo lilifungwa na Mzambia, Obrey Chirwa baada ya kosa la kwanza la kipa huyo Mghana ambaye kabla ya mechi hiyo alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa Azam FC wa mwezi uliopita.

Katika mechi hiyo, Azam FC walipata bao mapema kabisa katika dakika ya 3 lakini Yanga ikasawazisha kabla ya kupata la ushindi kupitia kwa Gadiel.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic