January 24, 2018



Straika nyota wa Simba, John Bocco amefunguka kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Masoud Djuma aliwapa sumu ya kuwamaliza wapinzani wao Kagera Sugar katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Bocco aliisaidia Simba kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar baada ya kuifungia bao moja, ambapo ushindi huo unaifanya Simba kukwaa kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 32 mbele ya Azam FC wenye pointi 30 katika nafasi ya pili.

Bocco mwenye mabao matano katika ligi kuu amesema kuwa, Djuma aliwapa maneno na mbinu za kuifunga Kagera Sugar katika vyumba hivyo baada ya kuona kwamba wamebanwa na kushindwa kufunga bao hadi kipindi cha kwanza kinaisha.

“Kikubwa tunashukuru kwamba tumepata pointi tatu kwenye mchezo huu dhidi ya Kagera Sugar ambao ulikuwa mgumu kwani wapinzani wetu walicheza kwa kukamia kwa muda wote na utaona hadi tunakwenda mapumziko hatukuwa tumepata bao lolote lile.

“Baada ya kuona hivyo wakati tupo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko, kocha alitupa maneno na mbinu za kuweza kufunga na kweli baada ya kufuatisha tukafanikiwa kupata mabao yale mawili ambayo yametufanya tuwe kileleni mwa msimamo, lengo ni kuendelee kufunga ili tutwae ubingwa,” alisema Bocco.


Katika mchezo huo, Bocco aliweka rekodi ya kumfunga kipa Juma Kaseja mabao 10 tangu walipokutana, akiwa mmoja wa washambuliaji waliomfunga kipa huyo mabao mengi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic