Kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali, amesema yupo kwenye mikakati mikali ya kumpika upya kipa namba moja wa timu hiyo, Rostand Youthe ili aje kuwa bora zaidi langoni tofauti na alivyo sasa.
Pondamali amesema kuwa anaanza kumpa mazoezi makali kipa huyo baada ya kuonekana uwezo wake upo chini tofauti na makipa waliomtangulia, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustapha ‘Barthez’.
Mbali na Rostand, pia Ramadhan Kabwili na Beno Kakolanya nao wamekuwa wakipewa mazoezi makali kuhakikisha wanaisaidia Yanga kufikia malengo.
“Taratibu naendelea kuwanoa makipa wangu kuhakikisha wanakuja kuwa bora kama wale waliotangulia.
“Hivi sasa si muda wa kuhoji sana ubora wa makipa wangu kama Rostand kwa sababu naendelea kuwanoa, lakini wakishakaa sawa, wenyewe mtawashangaa kama ilivyokuwa kwa Dida na Barthez naamini kuwa watakuwa bora siku siyo nyingi,” alisema Pondamali.
Rostand ambaye ameidakia Yanga kuanzia mwanzoni mwa msimu huu tayari amesharuhusu mabao saba kwenye ligi kuu hadi sasa.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment