January 1, 2018




Timu ya Simba, imeonekana kuwa na rekodi nzuri kila ikicheza na Ndanda FC kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara tangu msimu wa 2014/15 ambapo Ndanda ndiyo ilipanda daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

Simba ambayo hivi sasa inaongoza ligi ikiwa na pointi 26, juzi Jumamosi iliifunga Ndanda mabao 2-0 na kuifanya timu hiyo kushinda mchezo wake wa saba mfululizo katika michezo saba ya ligi kuu waliyokutana.
Ipo hivi; Katika msimu wa 2014/15, matokeo yalikuwa hivi; Ndanda 0-2 Simba mabao yakifungwa na Dan Sserunkuma na Elias Maguri. Mchezo ulipigwa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara. 

Ziliporudiana Uwanja wa Taifa jijini Dar, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na Jonas Mkude, Ramadhan Singano ‘Messi’ na Said Ndemla.

Msimu wa 2015/16, katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, matokeo yalikuwa Ndanda 0-1 Simba, bao lilifungwa na Ibrahim Ajib. Katika Uwanja wa Taifa ikawa hivi; Simba 3-0 Ndanda. Mabao yalifungwa na Mwinyi Kazimoto na Hamisi Kiiza alifunga mabao mawili.
2016/17 Simba ikicheza Uwanja wa Taifa, ikaibuka na ushindi wa mabao 3-1 yalifungwa na Laudit Mavugo, Frederick Blagnon na Shiza Kichuya, huku lile la Ndanda likifungwa na Omary Mponda. Zilipocheza kule Mtwara, Simba ikashinda tena 2-0 kwa mabao ya Mzamiru Yasin na Mohammed Ibrahim, kabla ya juzi John Bocco kufunga mabao mawili na kuipa ushindi wa mabao 2-0 timu yake ya Simba.

Akizungumzia hali hiyo, Ofisa Habari wa Ndanda, Idrisa Bandari, amesema: “Namna ambavyo tumekuwa tukijipanga na aina ya matokeo tunayoyapata yanatuumiza sana, kikubwa tunakubali matokeo na tunajipanga kwa michezo inayokuja.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic