January 1, 2018


Mshindi wa droo ya 56 ya promosheni ya Shinda na SportPesa inayoendeshwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya SportPesa Tanzania, Iddi Ndondole (28), mkazi wa Makambako amejishindia bajaji aina ya TVS King Deluxe.

Akizungumzia ushindi wake, Ndondole alisema: “Kusema ukweli nilifundishwa kucheza na mjomba wangu Brison Pascal, haswa kwenye zile hatua za mwanzo za kujisajili na baada ya hapo nikawa nacheza mwenyewe tu.

“Mara ya kwanza nilishinda shilingi elfu tano, mara ya pili nilishinda shilingi elfu ishirini na sita na mara ya tatu nilishinda shilingi elfu hamsini, kwa kweli siku hiyo nilifurahi sana hadi nikanunua kuku ili mimi na mke wangu tule siku hiyo.

“Siku chache baadaye nikiwa naendelea na safari yangu ya kubashiri nikapigiwa simu na mdada anayeitwa Happyness Wandela akinitaarifu kwamba nimejishindia bajaji aina ya TVS KING kutoka SportPesa aisee sikuamini kama ni mimi nimeshinda, nilikuwa shambani nalima nikaacha nikawahi nyumbani kwenda kumpa taarifa mke wangu naye nilimkuta anakula.”






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic