January 19, 2018



Yanga imeonekana kupania kufika mbali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutuma baadhi ya wawakilishi nchini Shelisheli kwa ajili ya kuwaangalia wapinzani wao, St Louis.

Kauli hiyo, aliitoa kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa muda mfupi mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC ambayo ilimalizika kwa suluhu.

Yanga wanatarajiwa kuanza kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi wapinzani wao St Louis kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mnamo Februari 27 kisha kurudiana ugenini.

“Tahadhari muhimu tunapoelekea katika michuano hii mikubwa Afrika imeshaanza kuchukuliwa, tumeanza mapema mikakati hiyo ya kutuma wawakilishi wetu watakaoifuatilia kwa ukaribu St Louis kwa kujua mbinu wanazozitumia wakiwa uwanjani, pia wachezaji hatari wa kuchungwa.

“Kingine ni kwenda kuandaa mazingira ya hoteli kabla ya timu kwenda huko katika mechi ya marudiano kama unavyofahamu fitna zinakuwa nyingi katika michuano hii,” alisema Nsajigwa. 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic