February 22, 2018



Na George Mganga

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, amesema kuwa anatambua uwepo wa mchezaji kutoka Tanzania anayekipiga barani Ulaya.

Infantino amemtaja mchezaji Mbwana Samatta, ambaye anaichezea KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji.

Rais huyo ameeleza kuwa anamfahamu mchezaji huyo kuwa anaitumikia Genk, wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka FIFA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Infantino aliongoza mkutano huo wa FIFA, ambao ulikuwa maalum kwa ajili ya kuendeleza soka la vijana, mipango ya kuvisaidia vilabu, pamoja na upigaji vita rushwa katika soka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic