February 3, 2018








Kikosi cha Simba kilipata mwaliko wa heshimu kutoka kwa Balozi wa Uturuki nchini, Ali Dovutoglu.

Kikosi kizima cha Simba kilifika nyumbani kwa balozi huyo na kufanya ziara maalum nyumbani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata chakula cha usiku.

Wachezaji wa Simba wakiongozwa na benchi lao la ufundi pamoja na mwanachama maarufu Mohamed Dewji ambaye amepitishwa kuwekeza katika klabu hiyo walifika nyumbani kwa balozi huyo. 








2 COMMENTS:

  1. Waturuki mafundi hasa katika masuala ya miundo mbinu nnaimani katika uhusiano huu mzuri wa Club ya Simba na Balozi itakuwa chachu ya Simba kujikita zaidi katika kutatua suala la tatizo la muda mrefu la miundo yake hasa tatizo la uwanja.

    ReplyDelete
  2. Simba sasa wanaingia kwenye anga za juu. Kualikwa na Balozi wa nchi ni heshima kubwa. Ni muhimu kuenzi kuheshimika kwenu huko na kutumia mahusiano hayo mazuri kuleta maendeleo zaidi kwenye klabu. Vizuri pia mkafanya ziara ya mafunzo huko Uturuki na kucheza mechi za kirafiki lakini pia mkazialika timu za Uturuki kuja nchini kucheza mechi za kirafiki. Mtunze heshima zenu nje na ndani ya uwanja. Hongereni sana wekundu wa msimbazi. Hiyo ndiyo Simba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic