February 23, 2018



Na George Mganga

Baada ya kuwasili nchini ikitokea Djibout, klabu ya Simba inaanza mazoezi leo kwa ajili ya kuiwinda Mbao FC, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Simba itaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani, ambao upo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar  es Salaam.

Kikosi hicho kinaanza mazoezi hayo leo, mara baada ya mechi ya Kombe la Shirikisho Africa dhidi ya Gendarmarie Nationale FC, ambayo waliifunga kwa jumla ya mabao 5-0 na kufanikiwa kusonga mbele.

Mechi hiyo ya Simba dhidi ya Mbao, itachezwa katika Uwanja wa Taifa, Jumatatu ya February 26 2018.

1 COMMENTS:

  1. Picha hiyohiyo tu kila habari ya Simba? Huna picha nyingine ambayo hujaitumia?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic