February 23, 2018



Kiungo mshambuliaji wa Everton, Wayne Rooney, ameeleza sababu ya yeye kurejea Everton na si kwenda China.

Rooney amesema wachezaji wengi wanaocheza katika Ligi Kuu Uingereza hukimbilia katika bara la Asia, pale umri unapowatupa mkono au wanapohitaji fedha.

Kiungo huyo amerejea Everton kutokana na namna ilivyomkuza kabla hajajiunga na Manchester United ambayo imetwaa taji la ligi mara 20.

Rooney amesema kuwa amerudi Everton ili kuwaonesha mashabiki wake kuwa bado anaweza, na atajihidi kuonesha mchango wake ili timu iweze kusonga mbele.

Vilecile ameongezea kwa kusema kuwa ilikuwa maamuzi sahihi kwake kufanya hivyo, anaamini ndani ya miaka miwili, mpaka mitatu ijayo, timu itafika mbali kimafanikio.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic