March 8, 2018


Na George Mganga

Licha ya ushindi kiduchu ilioupata dhidi ya Mwadui FC kutoka Shinyanga jioni ya leo, Azam FC imeishusha Yanga mpaka nafasi ya pili.

Azam imepanda kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kufikisha alama 41 dhidi ya Yanga yenye pointi 40 ambayo ina kiporo cha mchezo mmoja utakaopigwa kesho dhidi ya Kagera Sugar.

Bao pekee la Azam lililoipa nafasi ya kubeba pointi tatu muhimu, lilifungwa mapema zaidi kwenye dakika ya 5 ya mchezo na mchezaji Yahya Zayd

Bao hilo pekee lilidumu kwa dakika zote 90 na mpaka mwisho wa mchezo, hakukuwa na mabadiliko kwenye ubao wa matokeo.

Matokeo mengine katika mechi za leo ni Jombe Mji imepoteza ugenini mjini Iringa dhidi ya Lipuli FC kwa mabao 2-1, mabao ya Lipuli yakifungwa na Jerome Lambele (8') na Adam Salamba (77'). Bao pekee la Njombe Mji lilifungwa na David Obash (33').

Vilevile kule Shinyanga kwenye uwanja wa CCm Kambarage, Stand United ilikaribisha Tanzania Prisons, na matokeo yalimalizika kwa suluhu ya 0-0.

Na katika uwanja wa Majimaji, Majimaji FC imezidi kujiwekea mazingira mabaya ya kushuka daraja, baada ya kupoteza dhidi ya Ndanda FC kwa bao 1-0, bao likifungwa na John George.

1 COMMENTS:

  1. Mechi ya Azam na Mwadui nimeiangalia. Timu zote zimecheza vizuri. Azam amepata ushindi wa goli 1-0 nalilofunga kijana Yahaya Omari Zayd. Baada ya kufunga goli akafungua bukta yake kiunoni akatoa karatasi iliyokuwa imeandika ujumbe fulani akaenda golini kufungua na kushangilia na wenzie. Mimi nalaani kitendo hicho. Nilitegemea Refarii angempa kadi ya njano. Hivi karatasi ile ilipitaje bila kukaguliwa? jibu aliificha. Je angeweka upupu au unga wa sumu ya kumwagia mchezaji mwenzie au refa? Hapakuwa na sababu ya kufanya vile. Je wachezaji wote wafiche karatasi za namna ile na wanapofunga goli wazitoe? Zayd mchezaji mzuri sana lakini kitendo hiki kina madhara kwenye maadili ya mpira asifanye hivyo. TFF iangalie mambo haya na kuyazuia kabisa vinginevyo ipo siku yataleta madhara uwanjani pasipo kutegemea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic