MCHEZO WA SIMBA NA NJOMBE WASOGEZWA MBELE, SASA KUPANGIWA TAREHE NYINGINE
Na George Mganga
Mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba SC dhidi ya Njombe Mji imesogezwa mbele ili kuipa nafasi Simba ya kufanya maandalizi ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Masry.
Awali ratiba ya ligi ilionesha Simba walipaswa kukipiga na Njombe Mji, baada ya kucheza na Mtibwa Sugar Jumapili ya wiki hii kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi, sasa mechi hiyo sasa itapangiwa tena tarehe nyingine ili kuipa nafasi Simba ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, itakayopigwa Misri Machi 17 2018.
Katika mchezo wa marudiano, Simba watapaswa kushinda bao 1-0 au zaidi ya moja ili iweze kusonga mbele kwenye mashindano haya.
Na katika msimamo wa ligi, bado Simba ipo kileleni ikiwa imecheza michezo 20.
Mechi ya Azam na Mwadui nimeiangalia. Timu zote zimecheza vizuri. Azam amepata ushindi wa goli 1-0 nalilofunga kijana Yahaya Omari Zayd. Baada ya kufunga goli akafungua bukta yake kiunoni akatoa karatasi iliyokuwa imeandika ujumbe fulani akaenda golini kufungua na kushangilia na wenzie. Mimi nalaani kitendo hicho. Nilitegemea Refarii angempa kadi ya njano. Hivi karatasi ile ilipitaje bila kukaguliwa? jibu aliificha. Je angeweka upupu au unga wa sumu ya kumwagia mchezaji mwenzie au refa? Hapakuwa na sababu ya kufanya vile. Je wachezaji wote wafiche karatasi za namna ile na wanapofunga goli wazitoe? Zayd mchezaji mzuri sana lakini kitendo hiki kina madhara kwenye maadili ya mpira asifanye hivyo. TFF waangalie mambo haya ipo siku yataleta madhara uwanjani.
ReplyDeletesikuiona lakn nadhani upo sahihi, shida ya vijana weu wanakua hawajapitia academy za soka na kufundwa vilivyo kuhusu soka miiko na maadili yake na unakuta kajulikana na timu ukubwani..............ingawa inaweza isimguse Zayd moja kwa moja lkn wapo wengi wa kaliba yake .......ni funzo na tuendelee kuwalea vijana wetu kimpira na kisaikolojia
DeleteInabidi aulizwe kitendo hicho amekifanya kinamaanisha non,angelificha bastola hali ingelikuwaje?tff mcifumbie macho mbna ulaya hatuyaoni hayo?
ReplyDeleteSikuuulizwa tu nahatua achukuliwe
ReplyDelete