BAADA YA AL MASRY KUVURUGA RATIBA YA SIMBA LIGI KUU, SASA YAPANGIWA TAREHE HIZI KUKIPIGA NA NJOMBE PAMOJA NA MTIBWA
Michezo miwili iliyokuwa imehairishwa Njombe Mji dhidi ya Simba SC pamoja na Mtibwa Sugar Vs Simba SC sasa imepangiwa tarehe ya kuchezwa.
Tarehe 3 April 2018 kikosi cha Simba kitashuka uwanjani kucheza dhidi ya Njombe Mji katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Kikosi hicho pia kitasafiri mpaka Morogoro kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri mkoani humo tarehe 8 April 2018.
Mechi hizo zimepangiwa tarehe hizo baada ya kupewa nafasi ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masy SC
Simba waliomba ratiba hiyo isogezwe mbele ili kupata nafasi ya kufanya maandalizi dhidi ya mchezo huo, kabla ya safari yao kuelekea Misri.
0 COMMENTS:
Post a Comment