March 4, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha Genk usiku wa jana kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 kikiwa ugenini dhidi ya Waaslan-Beveren, mechi ikichezwa katika Uwanja wa Freethiel nchini Ubeligiji.

Katika mchezo huo, Mtanzania Mbwana Samatta hakuwa katika kikosi cha kwanza kwa kuanzia benchi, akichukua nafasi ya Mgiriki Nikolaus Karelis katika dakika ya 70.

Bao la Genk ugenini lilifungwa na mchezaji kutoka Gambia, Omar Colley katika dakika ya 68 na kudumu kwa dakika zote 90.

Samatta amecheza mechi hiyo baada ya kukosa mchezo uliopita dhidi ya Antwerp iliyopigwa katika Uwanja wa nyumbani na kushinda mabao 4-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic